Dirisha dogo la usajili linaweza kupita na hawa

0
1416
Football article
Football article

Andrew Vicent, Mzamiru Yassin, Mohamed Issa, Hassan Dilunga wapo Njia panda katika dirisha dogo la usajili mwezi Desemba 15, 2019.

Wachezaji hao na wengine wanaweza kuondoka kutokana na mikataba yao kumalizika, na baadhi yao kushindwa kuonyesha uwezo.

ANDREW VICENT ‘DANTE’
Ameweka wazi kuwa anataka kuondoka Yanga atakapolipwa fedha zake za usajili anazodai zinazokadiliwa kufikia Sh47 Milioni.
Mkataba wake unaisha mwishoni mwa msimu na anaweza kuondoka Kama mchezaji huru Baada ya msimu wa Ligi kuu Tanzania bara.

HASSAN DILUNGA.
Amekuwa katika kiwango kikubwa mno tangu amejiunga na Simba katika msimu uliopita akitokea Mtibwa Sugar.
Uwezo wake wa kubadilisha mchezo umekuwa chachu ya Aussems kumtumia kama mbadilishaji mchezo kwani anajua kucheza vizuri na muda.
Msimu huu ni wa mwisho kwake akiwa na Simba.

MZAMIRU YASSIN
Mzamiru anamaliza mkataba wake msimu huu akiwa na Simba. Kwa kiwango Chake Ni wazi Simba wanamuhitaji Sana kiungo huyu.

MUDATHIR YAHYA
Amebakiza miezi sita tu akiwa na Azam Fc, amegeuka kuwa nguzo katika eneo la kiungo. Azam wanaweza wakamkosa kwa msimu ujao baada ya kuonyesha kiu ya kutaka kusakata soka la kulipwa nje ya nchi.

DAVID MWANTIKA
Kukosa kwake nafasi katika kikosi cha Azam fc inaweza ikawa tiketi ya yeye kutoendelea kusalia Azam Fc.

MOHAMED ISSA ‘MO BANKA’
Mo Banka alisaini mkataba wa miaka miwili katika kikosi cha Yanga. Hakuweza kuitumikia hiyo mwanzoni mwa msimu uliopita lakini msimu huu ukimalizika anakuwa mchezaji huru.

IDD KIPAGWILE
Tangu msimu uliopita amejikuta akiwa katika wakati mgumu kwenye kikosi cha Azam.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here