Ditram Nchimbi hana mpango wa kuendelea na ligi Kuu Tanzania

0
469

Mshambuliaji chipukizi wa Taifa Stars, Ditram Nchimbi anasema hana mpango wa kuendelea kucheza ligi Kuu Tanzania bara. Ditram Amesema hayo pindi mkataba wake na Azam FC ukifika tamati mwisho wa msimu huu atatafuta timu Nje ya Tanzania.

Nchimbi ambaye bao lake la ushindi kwa Stars dhidi ya Sudan liliipeleka Stars kwenye fainali za CHAN baada ya miaka tisa. Ameanza kutajwa kutakiwa na klabu kubwa za Simba, Yanga pamoja na Azam.

Ditram yupo kwa mkopo Polisi Tanzania amekuwa katika kiwango kizuri kiasi cha kuitwa kikosi cha Stars chini ya kocha Etienne Ndayiragije.

“Mkataba wangu na Azam unamalizika Juni. Wamenipigia niongeze mkataba lakini sifikirii kufanya hivyo kwa sasa. Natamani sana kucheza nje,” alisema Nchimbi.

“Unajua nimecheza klabu tano za Ligi Kuu na sasa nataka kucheza nje. Kwa hapa nchini mimi naona imetosha aisee,” aliongeza Nchimbi.

Nchimbi ni mchezaji wa kwanza msimu huu kupiga ‘hat- trick’ katika pambano dhidi ya Yanga kwenye ligi kuu Tanzania bara.

“Ni kweli lakini kama nilivyosema, naweza kuacha mkataba wangu ufike mwisho nikacheze zangu nje,” amesema Ditram Nchimbi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here