Juma Kaseja Amkingia Kifua nahodha Mbwana Samatta.

0
349

Nahodha msaidizi wa Taifa Stars, kipa Juma Kaseja amemkingia kifua nahodha mkuu na straika tegemeo wa timu hiyo, Mbwana Samatta.

Juma Kaseja anamkingia Mbwana Samatta Kifua kutokana na shtuma anazopewa za kutojituma kikosini cha timu ya Taifa.

Kaseja amewaambia wanahabari kua haoni kama ni jambo sahihi kupewa mzigo mmoja bali iwe kwa timu nzima imepoteza mchezo huo.

“Sioni kama ni jambo sahihi imepoteza timu nzima, isitoshe ana mchango mkubwa Stars endapo kama siku hiyo hakuwa vizuri yeye binadamu huwezi kujua nini kilimkuta,” amesema.

Juma Kaseja anayecheza Katika Klabu ya KMC inayoshiriki Ligi kuu Tanzania Bara, ametoa Kauli hiyo juu ya Mbwana Samatta.

Mashabiki wa soka Nchini waliuliza kwanini Samatta hajitumi Kama anavyojituma Katika Klabu yake ya KRC GENK ya Nchini Ubelgiji.

Anasema licha ya kupoteza kwa mabao 2-1 dhidi ya Libya ana amini watafanya vizuri kwenye mechi ambazo zipo mbele yao.

“Ni kweli tunakubali kupokea lawama ingawa hatupendezewi nazo, ila ni vyema kuheshimu soka, kocha alituma plani ile ila bahati haikuwa upande wetu,”

“Lazima tufanye maandalizi kulingana na timu ambayo tunakwenda kucheza nayo, tumeteleza sasa tuungane kwa pamoja tuangalie mbele,”.

Taifa stars Inakua ya Tatu Katika kundi J lakufuzu fainali za Mataifa ya AFRIKA ( AFCON) 2021 Nchini Cameroon.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here